Mwantika aitwa Stars kuziba pengo la Morris

Wednesday June 19 2019

 

By CHARITY JAMES

Dar es Salaam. Beki wa Azam FC, David Mwantika amerudishwa nchini Misri tayari kuungana na kikosi cha Taifa Stars kuzipa pengo la Aggrey Morris  aliyeumia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri.

Mwantika ni miongoni mwa wachezaji waliopunguzwa katika kikosi hicho akiwa sambamba na beki Abdi Banda.

Chanzo cha ndani kutoka katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kililiambia Mwanaspoti kuwa Mwandika ameondoka nchini usiku huu kwaajili ya kuziba lengo la Morris.

"Mwandika yupo njiani anaelekea Misri kuungana na Stars kwani Morris anaweza akakosa mashindano kutokana na kukubwa na majeraha," alisema.

Taifa Stars itaanza harakati zake za katika mashindano ya Afcon 2019 kwa kuwavaa Senegal katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi C Juni 23 kwenye Uwanja wa Cairo.

Advertisement