NBA yaamua kukaukia vyombo vya habari China

Friday October 11 2019

Shanghai, China (AFP).Chama cha Mpira wa Kikapu cha Marekani (NBA) leo Ijumaa kimesema kuwa kimefuta shughuli zaote za vyombo vya habari kwa ajili ya mechi zilizosalia za kujiandaa kwa msimu, kikisema kumetokea "utata usiomithilika" kuhusu maandamano ya Hong Kong na uhuru wa kujieleza.
"Tumeamua kutokuwa na shughuli na vyoombo vya habari kwa ajili ya timu zetu kwa muda wote uliosalia wa ziara yetu nchini China," ilisema NBA katika taarifa yake.
"Wamewekwa katika hali tata na ambayo haijawahi kutokea wakati wakiw anje na naamini haitakuwa haki kuwaomba kuelezea mambo haya kwa wakati."
Mwakilishi wa NBA aliiambia AFP kwamba mechi ya pili kati ya mbili zilizopangwa kufanyika China baina ya Los Angeles Lakers na Brooklyn Nets Jumamosi usiku katika mji wa Shenzhen ulio kusini, bado itafanyika kama ilivyopangwa.
Timu hizo mbili zilicheza mechi yao ya kwanza mjini Shanghai Alhamisi.
Mapema kampuni za utangazaji ziliachana na mpango wa kurusha moja kwa moja matangazo ya mechi mbili za nchini China kupinga vitendo vya viongozi wa NBA.
Mechi hizo za kila mwaka nchini China zimekumbwa na utata tangu kiongozi wa Houston Rockets kueleza kuunga mkono waandamanaji wa harakati za kidemokrasia wanaoendelea na maandamano Hong Kong na kusababisha hamaki mbaya kutoka China.
Mzozo huo umesababisha wadhamini wa NBA nchini China kuvunja mahusiano kupinga kitendo hicho na kuibua mzozo zaidi katika uhusiano baina ya China na Marekani baada ya mwanasiasa maarufu wa Marekani kuitaka NBA iachanae na shughuli zake zote nchini China.
NBA ilishafuta mlolongo wa matukio ya kutangaza ligi hiyo na mikutano na vyombo vya habari mjini Shanghai wakati mzozo huo ukikua.

Advertisement