Neymar alilia kwa siku mbili baada ya kuumia

Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa nyota huyo wa Brazil kupata jeraha sehemu ileile aliyoumia mapema mwaka jana na kulazimika kufanyiwa upasuaji.
Neymar "alilia kwa siku mbili" baada ya kuumia mguu wa kulia kwa mara ya pili mwezi Januari, alikiambia kituo cha televisheni cha Brazil kwa mujibu wa vipande vya mahojiano vilivyorushwa jana Jumanne.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anayeichezea klabu ya Paris Saint-Germain aliona kuwa kupata tena jeraha kwenye mfupa alioumia Februari mwaka 2018 ambako kulilazimisha upasuaji mwingine, kulikuwa hatari kwake.
"Hii ni mbaya zaidi. Mara ya kwanza nilipoumia nilisema kwamba nitalazimika kufanyiw aupasuaji, ni lazima ufanyike mapema iwezekanavyo. Sikusikitika sana," alikiambia kituo cha televisheni cha Globo TV.
"safari hii, imekuwa ngumu zaidi. Nililia kwa siku mbili nyumbani."
Jeraha hilo alilopata katika mechi ya Kombe la Ufaransa ambayo timu yake ilishinda dhidi ya Strasbourg Januari 23, limemfanya mshambuliaji huyo wa Brazil kukaa nje kwa wiki kumi. PSG inatumaini kuwa atarejea uwanjani kabla ya mechi za robo fainali za Ligi ya mabingwa Afrika mwezi Aprili.
safari hii, jopo la madaktari wa klabu hiyo limeamua kumfanyia tiba ya kawaida badala ya upasuaji mweingine.
Mwaka jana, Neymar alikaa nje kwa miezi mitatu baada ya kufanbyiwa upasuaji na kurejea katika muda muafaka kabla ya fainali za Kombe la Dunia.
Mahojiano kamili na Globo TV yanatarajiwa kurushwa Machi 3. AFP