Niyonzima: Hii Sevilla bonge ya funzo kwetu

Friday May 24 2019

 

By THOMAS NG'ITU

Dar es Salaam. Matokeo 4-5 waliyopata Simba dhidi ya Sevilla yamewapa somo wachezaji wa mabingwa hao wateule wa Ligi Kuu Bara.

Baada ya mchezo kumalizika kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima alisema katika mchezo huo wamejifunza vitu vingi ambavyo anaamini vitawasaidia.

"Kuna vitu tofauti ambavyo wametuonyesha, mimi na wao tunapiga mpira tofauti kwahiyo kuna namna ambayo nimejifunza kupitia wao," alisema.

Aliongeza matokeo waliyopata ni sehemu ya mchezo kutokana na timu hiyo kuwazidi kiuwezo.

Naye kipa Deogratius Munish alisema magoli waliyofungwa haimaanishi kutetemeka kwani hata Sevilla nao walifungwa.

"Matokeo haya sio kama tulikuwa tunatetemeka, lakini kilichotokea ni kwamba mchezo tu ndio maana wenzetu nao wamefungwa," alisema Dida.

Advertisement

Advertisement