Nyoni arejea kikosini Simba, awekwa kikao

Wednesday March 13 2019

 

By THOMAS NG'ITU

Dar es Salaam. Beki wa Simba, Erasto Nyoni amerejea katika kikosi hicho baada ya kukaa nje kwa muda mrefu akisumbiwa na majeraha ya goti.

Katika mazoezi yanayofanyika kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Erasto aliwekwa kikao na benchi la ufundi takribani dakika tano.

Kikao hiko kiliongozwa na kocha Patrick Aussems na msaidizi wake Dennis Kitambi na baada ya hapo walianza progamu zao za kawaida.

Kurudi kwa Nyoni katika kikosi cha Simba unarudisha matumaini kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi huku kikosi hiko kikiwa kinamkosa Jonas Mkude katika mchezo dhidi ya As Vita baada ya kuwa na kadi mbili za njano.

Nyoni aliumia goti katika mashindano ya Mapinduzi Cup na kumfanya akosekane katika kikosi cha Simba kwa miezi mitatu.

Advertisement