Nyota Juventus augua moyo ghafla

Muktasari:

  • Semi Khadira atakosa mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid, baada ya kubainika na tatizo la moyo.

Rome, Italia. Nyota wa Juventus Semi Khedira atakosa mechi ya leo dhidi ya Atletico Madrid baada ya kubainika na tatizo la moyo.

Khedira alifanyiwa uchunguzi wa afya jana jioni katika mazoezi ya Juventus ambako alibainika na tatizo hilo.

Taarifa ya awali imesema kiungo huyo nguli hana tatizo ambalo  litakuwa tishio kwa maisha yake ya soka na amebaki Italia.

Juventus ‘Kibibi Kizee’ cha Turin leo usiku itakuwa ugenini mjini Madrid katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, alijiunga Juventus mwaka 2010 akitokea Real Madrid alikosa mechi 102 na kufunga mabao sita.

Khedira amecheza jumla ya mechi 86 na kufunga mabao 21 katika kikosi cha Juventus.

Katika hatua nyingine, mshambuliaji Paulo Dybala atacheza leo  licha ya kukabiliwa na matatizo binafsi.

“Nataka nikwambie Paulo yuko fiti,” alisema kocha wa Juventus Maximillian Alegri.