Nyota zaidi kuondoka Arsenal, lakini mkakati waandaliwa

Muktasari:

Katika msimu wa usajili uliomalizika, vigogo hao wa London walinunua wachezaji kadhaa nyota kama Nicolas Pepe, lakini wengine wanamaliza mikataba yao muda si mrefu

Kunaweza kukawa na wachezaji zaidi watakaoondoka Arsenal kabla ya kumalizika kwa kipindi cha usajili barani Ulaya, anakiri Josh Kroenke, lakini klabu hiyo pia inapanga kuanza mazungumzo ya mikataba mipya na wachezaji muhimu pamoja na kocha Unai Emery wakati muda utakapofika.
Kipindi cha usajili ambacho kilikuwa na matukio mengi kilishuhudia Arsenal ikiingiza sura mpya nyingui, akiwemo winga aliyenunuliwa kwa dola milioni 87 milioni za Kimarekani, Nicolas Pepe.
Kukabiliana na waliowasili, wachezaji kadhaa pia wameondoka – ama kwa mkopo ama kwa uhamisho wa moja kwa moja.
Inawezekana klabu ikaruhusu wachezaji zaidi kabla ya siku ya mwisho ya usajili duniani iwapo wataonekana hawahitajiki.
Kronke, mjumbe wa bodi ya Arsenal na mtoto wa mmiliki wa klabu hiyo Stan, aliiambia BBC Sport alipoulizwa kuhusu wachezaji wanaoondoka kuwa anaweza kutofutiana na watendaji, lakini anajua kuna wachezaji ambao hawatapata nafasi.
“Nitatofautiana na wafanyakazi wanaohusika na uendeshaji wa soka, lakini najua majina machache yaliyokuja ambayo hayatapata muda mwingi wa kucheza msimu huu, kwa hiyo iwe kwa mkopo au uhamisho najua kuna mazungumzo yanaendelea. Nitaliacha hilo kwa wan aohusika na uendeshaji soka.”
Wakati akitegemea kuna watakaoondoka Emirates hivi karibuni, Kroenke anajua umuhimu wa kuhakikisha kuwa mali zenye thamani haziruhusiwi kuondoka.
Arsenal ina wachezaji kadhaa wanaoelekea kumaliza mikataba yao katika miaka ya karibuni, kuna kuna haja upande wao wa kuepuka kurudia kosa lolote.
“Kwa asilimia 100 hilo liko upande wa idara inayohusika na uendeshaji soka, lakini naweza kusema iwe tunafanya au la tutakuwa jasiri na wenye uamuzi na tutawasiliana vizuri na kuwa wakweli wakati wote," alisema Kroenke.
“Kwa hiyo kutokana na mtazamo wa mchezaji, kama ni habari nzuri au mbaya, nadhani kitu bora unachoweza kufanya ni kuwa mkweli kwa sababu muda wa uhamisho ni mdogo kulinganisha na muda wao wa kuwa katika kiwango cha juu. Kwa hiyo nitawaachia shughuli zote (watu wanaohusika na uendeshaji soka) kwa kuwa ni wazuri katika hilo.”
Mkataba mmoja ambao atahitaji kuushughulikia ni wa kocha mkuu, Emery, huku Kroenke akiwa amesharidhishwa na kazi iliyokwishafanywa hadi sasa na kocha huyo kutoka Hispania tangu mbadili gwiji, Arsene Wenger.
“Nadhani anafanya kazi nzuri, amefanya kazi nzuri na anafanya kazi kubwa,” alisema Kroenke.
“Kugeuza ukurasa kutoka kwa kocha gwiji kama Arsene - na si kwenye klabu ya Arsenal pekee bali soka la Ulaya - siku zote ni kazi ngumu na nadhani kama klabu tumelifanya kwa busara.