Okwi ashonwa nyuzi mbili

Muktasari:

  • Daktari wa Simba, Yassin Gembe amesema hali ya Okwi inaendelea vizuri.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi raia wa Uganda amechanika na kushonwa nyuzi mbili chini ya jicho upande wa kushoto.

 Okwi amepata majeraha hayo baada ya kugongana na beki wa kushoto wa Azam FC, Bruce Kangwa dakika ya 72, jambo lililopelekea atolewe na kupelekwa kwenye vyumba vya huduma ya kwanza.

 Daktari wa Simba, Yassin Gembe amesema hali ya Okwi inaendelea vizuri.

"Pamoja na majeraha hayo Okwi yupo vizuri na ataendelea na mazoezi kama kawaida,"alisema Gembe ambaye aliitibu pia Mtibwa Sugar miaka ya nyuma.

Amefafanua nyuzi mbili alizoshonwa Okwi si tatizo kwa sababu wanaye kocha mzuri wa viungo Mtunisia Adel Zrane.