Ole apanga kufanya uamuzi mgumu Manchester United

Muktasari:

  • Solskjaer alisema kuwa anafahamu nini anataka kufanya akitambua kuwa lazima kuwa karibu na timu kama Manchester City na Liverpool msimu ujao na kuifanya Manchesster United kuwa timu ya ushindani.

London, England. Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema ana kibarua kimoja kizito cha kukifumua kikosi cha Manchester United baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya England.

Baada ya kushinda mechi zake 10 kati ya 11 mara baada ya kuichukua timu, United imepoteza mechi nne kati ya tano chini ya Solskjaer.

Man United, ambayo ililala kwa West Ham iko nafasi ya sita, ikiachwa kwa pointi tatu na Tottenham huku ikiwa na mechi sita mkononi, huku kukiwa na wasiwasi wa kuikosa nafasi ya nne msimu huu.

Solskjaer alisema kuwa anafahamu nini anataka kufanya akitambua kuwa lazima kuwa karibu na timu kama Manchester City na Liverpool msimu ujao na kuifanya Manchesster United kuwa timu ya ushindani.

Tayari baadhi ya wachezaji akiwemo; Ander Herrera, Juan Mata, Antonio Valencia, Matteo Darmian, Marcos Rojo na Alexis Sanchez ni kati ya ambao wanaiacha klabu hiyo mwishoni mwa msimu huku Real Madrid ikimpigia hesabu Paul Pogba.

Msaidizi wa Solskjaer, Mike Phelan alisema kuna kila sababu ya kufanya uamuzi mgumu kwenye timu kama watu wanataka Manchester United irudi kwenye chati.

“Hakuna jinsi, lazima uamuzi mgumu ufanyike ili mambo yaende,” alisema Solskjaer. “Itakuwa ngumu lakini lazima kufumua kikosi.”

“Itakuwa kwa ajili ya kupata watakaobaki na watakaolazimika kupunguzwa. Huo ndio hasa mkakati uliopo. Tunataka wachezaji wa kutuvusha hapa, kutengeneza amani kwenye timu na ndicho kitakachotubeba.”

“Liverpool na Manchester City wako mbali sana na sisi kwa sasa na sisi tunacheza na Barcelona timu ambayo ina viwango vya ubora duniani. Kama nilivyosema, hakuna kuleana tena itakuwa uamuzi mgumu kwelikweli kukata wachezaji lakini lengo ni kupata mwelekeo mpya. Uamuzi utakuwa wangu, Mick na klabu.”

Alipoulizwa kama wachezaji wa Manchester United wanacheza kwa ajili ya kesho yao, alisema: “Ninaamini wanapambana na wanafanya vyema tangu nilipookuja. Kuna standadi fulani hapa ya wachezaji, lakini kwa mazingira yaliyopo, inatuweka pagumu kwa matokeo na viwango.

“Tunataka kuona wachezaji wakiingia na tukasema: ‘Nataka kuona haya na yanakuwa’. Unamwona Fred na Scott McTominay.

“Hicho ndicho tunachokitarajia kwa wachezaji. Wakati unashinda mabao 5-0 au ukiwa mbele kwa mabao 3-0, au kushinda mechi kwa mabao mengi inakuwa rahisi kwamba wachezaji wanaingia una uhakika wa ushindi.