PSG, Neymar haikijaeleweka kabisa huko

Tuesday July 9 2019

 

By ELIYA SOLOMON

Dar es Salaam. Vigogo wa PSG wamepanga kumchukulia hatua, nyota wao Neymar kwa kushindwa kujiungana wenzake kwa maandalizi ya msimu ujao.

Neymar ameweka wazi juu ya dhamira yake ya kutaka kuondoka nchini Ufaransa majira haya ya kiangazi kwa kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya FC Barcelona.

Nyota huyo yupo Brazil akishudia timu yake ya taifa ikitwaa ubingwa wa kombe la mataifa ya Amerika Kusini ‘Copa Amerika’ wakiitandika Peru kwa mabao 3-1.

Kutokana na majeraha yanayomsumbua, PSG walitaka Neymar awasili mapema zaidi kitu ambacho kimekuwa tofauti na kile kilichotokea.

Inadaiwa kuchelewa huko kwa Neymar kumetokana na nyota huyo kuhudhuria fainali ya michuano ya Red Bull Neymar Jr's Five.

Advertisement