Prisons yasaka watano wapya

Thursday July 12 2018

 

By Olipa Assa

Dar es Salaam. Kocha wa Prisons, Abdallah Mohamed 'Bares' amesema ataongeza wachezaji wapya watano huku wawili akiwatoa timu za Zanzibar.

Bares alifanya vema katika msimu ulioisha, kikosi chake kikimaliza nafasi ya nne, huku yeye akichukua tuzo ya kocha bora, jambo linalomfanya ajipange kwa msimu mpya.

"Kikosi changu hakihitaji marekebisho makubwa, ila tunajaribu kuziba mapengo ya waliondoka, ndio tupo kwenye mchakato huo na wawili nawaangalia kwa timu za huku.

"Ligi inayokuja itakuwa ngumu kutokana na usajili unaendelea na ndio maana na sisi tunataka tuongeze wasiozidi watano ambao watawaongezea nguvu waliopo," alisema.

 

Advertisement