Rais Magufuli akabidhiwa ramani ya uwanja wa Dodoma

Muktasari:

Makabidhiano hayo ambayo ni ufadhili wa Mfalme wa Morocco Mohamed VI  yamefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam mbele ya Rais John Magufuli

RAIS wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, John Magufuli leo Jumatano amekabidhiwa ramani ya uwanja mpya utakaojengwa jijini Dodoma ambao utakuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki kuanzia 85,000 hadi 10,005.

Makabidhiano hayo ambayo ni ufadhili wa Mfalme wa Morocco Mohamed VI  yamefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam mbele ya Rais Magufuli, Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane, Kiongozi wa Ujumbe kutoka Morocco Balozi Mohamed Methqal ambaye ni  Mkurugenzi mkuu wa Wakala wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Morocco.

Pia ujumbe wao, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi wasabi, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale na Balozi Zuhuru Bundala.

Kwa nje uwanja huo utakuwa na muonekano kama mlima Kilimanjaro hivyo kuzidi kupamba madhari ya mjii mkuu wa Tanzania mkoani Dodoma.

Huu utakuwa ni uwanja wa kwanza kwa ukumbwa hapa nchini ukifuatiwa na uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 60,000 ambao ni miongoni mwa viwanja bora Afrika Mashariki na Afrika.