Rais TFF, Karia atangaza kamati mpya kusimamia soka Tanzania

Muktasari:

Kamati zilizochaguliwa ni kamati ya Rufani za Leseni, Kamati ya Mashindano, Kamati ya Habari na Masoko pamoja na kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji.

Dar es Salaam.BAADA ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kutangaza jana kuvunja kamati ya waamuzi iliyokuwepo na kuunda mpya, leo pia imetangaza kamati zingine kwaajili ya kusimamia mpira wa miguu nchini.

Kwenye kamati zilizochaguliwa leo, aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya  Waamuzi iliyovunjwa jana, Salum Chama amechaguliwa tena katika kamati ya Mashindano akiwa kaimu Mwenyekiti kwenye kamati ya Mashindano.

Wakati huo huo aliyewahi kuwa Meneja wa klabu ya Azam Fc, Philip Alando amechaguliwa kuwa mjumbe katika kamati ya mpira wa Vijana.

Kamati zilizochaguliwa ni kamati ya Rufani za Leseni, Kamati ya Mashindano, Kamati ya Habari na Masoko pamoja na kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji.

Kamati ya Rufani inaundwa na Dk Damas Ndumbaro (Mwenyekiti), Dk Alex Mgongolwa (Makamu Mwenyekiti), Charles Matoke, David Kivembele na Robert Selasela.

Kamati ya Mashindano inaundwa Ahmed Mgoyi (Mwenyekiti), Saloum Chama (Makamu Mwenyekiti), James Mhagama, Patrick Kahemele, Fortunatus Kalewa, Shafih Dauda, Sara Chao, Said Tully na Ally Kamwe.

Kamati ya Habari na Masoko, Steven Mnguto (Mwenyekiti), Osuri Kosuri, Cyprian kuyava, Mgaya Kingoba, Dk Omar Saleh na Saleh Ally.

Kamati ya Tiba inaundwa na Dk Paul Marealle (Mwenyekiti),Dk Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk Norman Sabuni, Dk Lisobina Kisongo, Dk Eliezer Ndama, Dk Billy Haonga na Dk Violet Lupondo.

Kamati ya Ufundi, Vedastus Lufano (Mwenyekiti), Mrisho Bukuku (Makamu Mwenyekiti),  Ibrahim Masoud, Ally Mayayi, Michael Bundala, Jumbe Menye na Edibily Lunyamila.

Kamati ya mpira wa vijana, Khalid Abdallah (Mwenyekiti), Lameck Nyambaya (Makamu Mwenyekiti), Mohamed Aden, Nassib Mabroukh, Salim Kibwana, Vicent Majili, Kenneth Pesambili, Nick Magarinza na Philip Alando.

Kamati ya Leseni za klabu, Wakili Lyod Nchunga (Mwenyekiti), Wakili Emmanuel Matondo (Makamu Mwenyekiti), Sunday Kayuni, George Mayawa na Tumaini Mringo.

Huku kamati ya mwisho ikiwa Sheria na hadhi za wachezaji ambayo inaundwa na Mwanasheria Elias Mwanjala (Mwenyekiti), Said Soud (Makamu Mwenyekiti), Zakaria Hans Pope, Issa Batenga, Wakili msanifu Kondo na Said George.