Rasmi Mkwabi ajizulu Simba

Saturday September 14 2019

 

By KHATIMU NAHEKA

MWENYEKITI wa Simba Swedi Mkwabi amejiuzulu nafasi yake, klabu hiyo imethibitisha rasmi.
Taarifa iliyotolewa na Simba inasema Mkwabi amechukua uamuzi huo akitaja sababu moja katika kufikia maamuzi hayo.
Simba imesema Mkwabi amewasilisha barua yake katika uamuzi wake huo akisema anataka kupata muda zaidi wa kusimamia shughuli zake binafsi.
Aidha Simba imesema inamtakia kila la kheri Mkwabi huku ikimshukuru kwa muda alioitumikia nafasi hiyo.
Sambamba na hilo Simba imesema taratibu juu ya kujaza nafasi hiyo zitatangazwa baadaye.
Taarifa za kujiuzulu kwa Mkwabi zilivuma zaidi wiki iliyopita lakini Simba ilishindwa kuthibitisha.

Advertisement