Real Madrid kutumia dau la kufuru kumnasa Mbappe

Muktasari:

Taarifa zimedai Real Madrid imekubali kutoa dau kubwa ili kuhakikisha inapata saini ya kinara huyo wa mabao Ufaransa.

Madrid, Hispania. Real Madrid ipo tayari kuvunja rekodi ya dunia ya kutoa Pauni340 milioni kuipata saini ya mshambuliaji wa Paris Saint Germain (PSG), Kylian Mbappe.

Mbappe ni miongoni mwa wachezaji wanawindwa na Zinedine Zidane akitaka kumsajili katika majira ya kiangazi.

Mshambuliaji huyo amekuwa katika kiwango bora na anazivutia timu nyingi kubwa barani Ulaya.

Miongoni mwa mafanikio aliyopata Mbappe mwenye miaka 20 ni kuipa Ufaransa Kombe la Dunia mwaka.

Taarifa zimedai Real Madrid imekubali kutoa dau kubwa ili kuhakikisha inapata saini ya kinara huyo wa mabao Ufaransa.

Kwa muda mrefu Mbappe amekuwa akihusishwa na klabu za Hispania tangu akiwa na miaka 17 akicheza Monaco.

Kinda huyo ana rekodi ya kufunga mabao 67 na kutoa pasi za mwisho mara 31 katika mechi 104. Msimu huu anapewa nafasi ya kutwaa kiatu cha dhahabu.

Zidane aliwageukia Eden Hazard aliyemsajili akitokea Chelsea na Luka Jovic wa Eintracht Frankfurt majira ya kiangazi msimu uliopita.

Uhusiano baina ya Mkurugenzi wa Ufundi wa PSG Leonardo na Zidane umekuwa wa karibu katika siku za karibuni.