Ronaldo amwita Mourinho wakapige kazi Juventus

Muktasari:

  • Ronaldo, Mourinho ilidaiwa walikuwa na ugomvi ndiyo moja ya sababu ya kocha huyo Mreno kutimuliwa ndani ya kikosi cha Real Madrid.

Rome, Italia. Cristiano Ronaldo amesema anataka kufanya kazi na kocha Jose Mourinho katika kikosi cha Juventus.

Ronaldo anamtaka Mourinho kwa kuwa alifanya naye kazi vizuri walipokuwa Real Madrid.

Kauli ya Ronaldo imekuja muda mfupi baada ya Massimiliano Alegri kutangaza kuondoka Juventus.

Kocha huyo Mtaliano anahusishwa na mpango wa kujiunga na Chelsea kujaza nafasi ya Maurizio Sarri ambaye amekalia kuti kavu.

Ronaldo ana amini Mourinho ndiye mtu sahihi wa kutua kwa ‘Kibibi Kizee’ hicho cha Turin majira ya kiangazi.

Mshambuliaji huyo alipata mafanikio alipokuwa Real Madrid na alitwaa mataji matano ya Ligi Kuu ambapo msimu 2011-2012 ulikuwa bora zaidi kwa wawili hao.

Msimu huo ndio Real Madrid ilikuwa katika kiwango bora na kuwapiku watani wao wa hadi Barcelona.

“Unaweza kufanya kazi na Mourinho tena? Ndio kwanini isiwe hivyo,” alijibu Ronaldo alipohojiwa muda mfupi baada ya Alegri kumaliza mechi ya mwisho akiwa Juventus.

Ronaldo ametwaa ubingwa wa kwanza akiwa Juventus msimu huu akitokea Real Madrid.

Nguli huyo aliyejiunga na Real Madrid mwaka 2009 akitokea Manchester United, alifunga mabao 311 katika mechi 292 alizocheza katika kikosi hicho.