Samatta, Msuva wamsapraizi Amunike

Muktasari:

  • Kona hizo zilipigwa kutokea upande wa kulia alikuwa akipiga Kichuya huku washambuliaji wote wakiongozwa na Samatta wakitakiwa kufunga na viungo na mabeki wakizuia.

Dar es Salaam. Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania' Taifa Stars' Emmanuel Amunike ameonekana kupania  kuingamiza Uganda 'The Cranes' baada ya leo Jumamosi asubuhi kwenye Uwanja wa Boko Veterani na kukazania soka la kushambulia muda wote na kufunga mabao kutumia mipira ya faulo.
Amunike alikuwa akiwataka wachezaji wake kufunga mipira hiyo kupitia kwa Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Simon Msuva na Shiza Kichuya.
Samatta na Msuva walionekana kuwa vizuri zaidi katika kufunga mipira hiyo ya faulo ya moja kwa moja kwani katika mipira minne waliyopiga walifunga mara mbili.
Wakati Samatta, Ulimwengu, Msuva na Kichuya wakiwa sehemu ya kupiga faulo, Amunike alipanga ukuta  ulioongozwa na Rashid  Mandawa, Himid Mao, Kennedy Juma, Feisal Salum ili kuzuia.
Pia, walifanya mazoezi mengine ya kufunga kwa kutumia mipira ya Kona.
Kona hizo zilipigwa kutokea upande wa kulia alikuwa akipiga Kichuya huku washambuliaji wote wakiongozwa na Samatta wakitakiwa kufunga na viungo na mabeki wakizuia.
Upande wa kushoto, kona zilipigwa na Mudathir Yahaya.
Katika kufunga kwa kutumia mipira ya kona wachezaji wengi walishindwa kufunga na mipira hiyo kuokolewa na mabeki.