Sarri awachokonoa mashabiki Chelsea

Muktasari:

  • Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri amewapuuza mashabiki wa klabu hiyo waliomzomea katika mchezo dhidi ya Manchester United.

London, England. Maurizio Sarri amesema hajali  kuzomewa na mashabiki wa Chelsea, baada ya timu yake kufungwa na Manchester United.

 Sarri alizomewa na mashabiki wa klabu hiyo kwenye Uwanja wa Stamford Bridge baada ya Chelsea kuchapwa mabao 2-0 katika Kombe la FA.

Kocha huyo wa zamani wa Napoli, alisema anahofia matokeo ya uwanjani si kuzomewa na mashabiki.

Paul Pogba na Ander Herrera walipeleka kilio Stamford Bridge baada ya kufunga mabao hayo yaliyoipeleka katika robo fainali.

Licha ya kufungwa katika mchezo huo wa Kombe la FA, Chelsea ilifungwa na Bornamouth, Manchester City katika mechi mbili ambazo ilichapwa idadi kubwa ya mabao mwezi huu.

Kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane ametoa masharti ya kwa uongozi wa Chelsea kama inamtaka kujaza nafasi ya Sarri.