Senzo atangaza kikosi kazi chake Haji Manara ndani

Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa ametangaza safu yake ya uongozi yenye watu 12 huku Haji Manara akiendelea kupeta katika nafasi ya Afisa Habari.

Senzo ametangaza orodha hiyo mpya atakayokuwa akifanya nayo kazi atasaidiwa na Rispa Hatibu ambaye ni Mkurugenzi Msadizi, Dr Anold Kashembe ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji, Suleiman Kahumbi ni Mhasibu Mwandamizi.

Wengine ni Belinda Paul ambaye ni Meneja Miradi, Hamisi Kissiwa ni Meneja Mashindano, Haji Manara ataendelea kuwa Afisa Habari, Hashim Mbaga ni Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki pamoja na Abbas Ally ambaye ni Meneja/Mratibu wa Mipango ya Soka.

Wengine ambao wapo chini ya uongozi huo ni Rabi Hume ambaye ni Mratibu Habari na Mitandao ya Kijamii, Jacob Kimangano ni Msaidizi Kitengo cha Masoko na vyombo vya habari, Juma Matari ni Meneja Vifaa pamoja na Saidi Hassan Ahmed ambaye ni Msaidizi wa ofisi.

"Nitakuwa na watu nitakaofanya nao kazi ndani ya Simba katika nafasi tofauti" amesema Senzo