Serikali yatoa sababu kutokuwepo matangazo Afcon

Muktasari:

  • Waziri wa Habari, Dk Harrison Mwakyembe amewaambia waandishi wa habari sababu za kutokuwepo mabango ya matangazo na hamasa kuwa ni masharti magumu ya Fifa

Dodoma. Serikali imetaja sababu za kutoweka matangazo ya kuhamasisha kwenye mashindano ya soka ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 (Afcon Under 17) yaliyofanyika jijini Dar es  Salaam mwezi uliopita..

Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe amesema leo Ijumaa Mei 17, 2019 kuwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) liliweka masharti magumu.

"Hata pale uwanjani mliona walitoa mabango yote hata ambayo yalikuwepo lakini tumejifunza mambo mengi ambapo tunaweza kuandaa hata mashindano ya Kombe la Dunia sasa," amesema Mwakyembe.

Waziri huyo amesema katika mashindano ya wenye ulemavu matangazo yatakuwa mengi kila kona kwani hakuna masharti kwa kuwa yanafanyika kwa mara ya kwanza na kuchukua nchi chache ambazo haziwezi kutoa ugumu.

Kuhusu mashindano hayo ya walemavu amesema mipango iko vizuri na kuyaomba makampuni kujitokeza kuisaidia timu hiyo na kuwa waanze matangazo kuanzia sasa.

Kwa mujibu wa Mwakyembe, timu hiyo itaingia kambini kuanza kujifua lakini akasema kuna wabunge ambao wanafanya kazi ya uhamasishaji mkubwa.

Timu ya wabunge hao ni Riziki Lulida, William Ngeleja, Venance Mwamoto, Margareth Sitta na Amina Mollel

 

Mwisho,.....