VIDEO: Sevilla ‘full muziki’ kutua Dar es Salaam kesho

Muktasari:

  • Hii ni mara ya kwanza kwa Sevilla kucheza na klabu ya Tanzania, Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara

Dar es Salaam. Miamba ya Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’, Sevilla FC itawasili nchini kesho Jumanne saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba.

Sevilla inayodhaminiwa na Sportpesa mbali ya kucheza mechi hiyo dhidi ya Simba pia watafanya shughuli za kijamii pamoja na kliniki na mafunzo mbalimbali.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kimataifa ya La Liga, Oscar Mayo alisema katika ushindani wa kimataifa unakutana na dhamira ya LaLiga kuwa karibu na mashabiki wake.

“Mashabiki wetu wa Tanzania watapata furasa ya  kuangalia karibu  Sevilla FC inamaanisha kuwa ni fursa kubwa kwa kila mtu," alisema Mayo.

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Tarimba Abbas alisema kampuni yao  imeshirikiana na baadhi ya taasisi za soka za kubwa  ulimwenguni  baada ya kuna kuna haja ya  kuleta uzoefu  huu mkubwa  kwa Tanzania.

 "Ili kufurahia kuona moja ya klabu kubwa Ulaya, Sevilla FC. Kwa makubaliano yetu na LaLiga ambayo ni ligi bora duniani, tutaweza kuonyesha vipaji vyetu na kuboresha kiwango cha soka nchini," alisema Talimba.

 Alisema mechi hiyo ni sehemu ya mradi wa 'LaLiga duniani  ambao unalenga kueneza soka  la  Hispania kimataifa na  kueneza pia sera ya 'Marca España', kuleta karibu mashabiki wa  LaLiga na  kukuza klabu nje ya nchi yetu.

Hii itakuwa ni klabu ya pili Ulaya kufanya ziara Afrika Mashariki, baada ya mwaka 2017, Everton FC kucheza  na  Gor Mahia nchini Kenya, ingawa sio mara ya kwanza kwa  Sevilla kutua katika bara hili kwani  mwaka  2015  ilikuwa nchini  Morocco ambao ilicheza mechi ya kuajindaa na  LaLiga dhidi ya Hassania Union Sport d'Agadir.