VIDEO: Shabiki Mbao aingia amepanda punda uwanjani

Muktasari:

  • Hii ni mara ya kwanza katika Ligi Kuu kushudia shabiki akiingia uwanjani akiwa amepanda punda

Mwanza. Katika soka wanaamini shabiki ni mchezaji wa 12 kwa timu, katika mchezo katika ya Mbao na Yanga mashabiki wa timu hizo walionyesha uwezo wao.

Shabiki wa Mbao, Samuel Kitundu alitoa kali ya mwaka baada ya kuingia uwanjani akiwa amepanda Punda huku akishangiliwa kwa nguvu.

Hii ni mara ya kwanza katika Ligi Kuu kushudia shabiki akiingia uwanjani akiwa amepanda Punda.

Nguvu kubwa ya Mbao imeelekeza kwa mashabiki wake kutoka matawi mbalimbali jijini humo. Jambo la kuvutia zaidi ni mashabiki kutoka makundi ya Chungu na Mazombe ambao wanatarajiwa kuwasha moto wa ushangiliaji uwanjani hapo.

Imeshuhudiwa mambo mengi yakifanywa na mashabiki wa Yanga wakati wachezaji wakiingia vyumbani ikiwa ni kumwaga maji sehemu ya kupita bila kujua sababu za vitendo hivyo.