Shiboub anapotusahaulisha Niyonzima, Kotei

Thursday August 22 2019

 

By KHATIMU NAHEKA

Pale Simba kuna mfalme mpya ameingia ameanza kazi yake kwa kasi mbaya sana,anakichafua pia analeta burudani kwa mashabiki wa timu hiyo.

Majina yake ni Sharaf Shiboub kiungo mmoja ambaye muonekanbo wa mwili wake unakusahaulisha na mengi anayofanya ndani ya uwanja mtafute umwone.

Msudani huyu amesajiliwa na Simba msimu huu na wala wengi hawakuwa wanamjua mtu wan am na hiyo na hakuvuma alitua kimyakimya kisha akasajiliwa kwa mkataba wa mwaka mmoja pale Msimbazi.

Sishangai ujio wa Shiboub pale Simba kinachonishangaza ni wale wajuaji wenzangu ambao walikuwa wanapiga kelele sana kuachwa kwa James Kotei na hata Haruna Niyonzima.

Viungo wote wawili walikuwa Simba msimu uliopita na kila mmoja alikuwa na uimara wake wakati Niyonzima akiwa na ubora wake wa soka la burudani na pasi zake za madaha Kotei alikuwa na ugumu wake katika kiungo cha chini.

Walipotangazwa wanaachwa wawili hao kila mmoja aliongea lake hasa mashabiki waliona kama Simba inakwenda kupotea kwa kuwaacha watu hao wawili.

Advertisement

Kelele zikiendelea mbele anatua Shiboub tena anatoka kusikojulikana tena kimyakimya akatua Msimbazi na kuanza kazi.

Kuna kitu cga kujifunza hapa kwamba unaweza kuwa na mkate alafu licha ya kukusaidia kushiba lakini kuna wakati unahitaji chakula bora zaidi ya hicho ili uimarishe mwili.

Niliona Simba katika mechi zao mbili za ugenini za Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita hawakuwa na ubora kabisa katika sehemu ya ulinzi hawakuwa na watu kariba kama ya Shoboub katika kiungo cha ulinzi chake.

Soka la sasa hatua nzuri ya kujilinda ni kuweza kutunza mpira kupitia umiliki wako wa kukaa na mpira, pia mtu anayejua kuziba njia za mpira.

Kazi hizi Shiboub anazifanya tena kwa weledi mkubwa anapiga pasi na kutengeneza vyema nafasi na sio kujificha kwamba akitoa pasi kamaliza.

Uwezo mwingine bora anaotuletea ni kujua kufunga mabao mawili aliyowafunga Azam FC yanatosha kuwa elimu ni kiungo ambaye anatakiwa kuangaliwa vyema msimu uliopita.

Wakati Shiboub akifanya vitu nikawa nawatafuta wale wadau wenzangu wa Kotei na Niyonzima nikawaona wote tunafurahia pamoja kazi ya kiungo huyu na kusahau mijadala ya nyuma.

Tanzania yetu kuna makocha wengi na viongozi wengi ambao ukiwasikiliza unaweza kuwapa madaraka makubwa hakuna anayetaka kujipa subira wala kuweka akiba ya maneno katika kitu husika.

Hii imekuwa taswira yetu kubwa ambayo imekuwa ikitukosesha mambo mazuri kutokana na kuwalazimisha makocha na vuiongozi kufanya maamuzi ya mihemko na kupoteza mwendo sahihi wa taaisisi.

Hatuwezi kujadili mambo kwa nafasi badala yake tunamajadili vitu kwa kutumia majina na jinsi tunavyikuwa na mahaba na watu fulani.

Naona kabisa kama angetua Shoboub kisha kuwekwa hadharani kati yake na Niyonzima asajiliwe yupi siku hiyohiyo Msudan huyu tena kwa mwonekano wake angekuwa yuko kwao haraka sana.

Hakuna anayetaka kujua Simba imekutana na yapi mpaka kuamua kuachana na mtu kama Niyonzima licha ya kipaji chake kinachoheshimika.

Wapo wachezaji wengi wamefeli hapa kwetu kutokana na kujadiliwa uwezo wao katika muda mfupi kisha wqakaonekana hawakustahili, nani anawezsa kuamini Laudit Mavugo amekuwa mshambuliaji bora huko Zambia katika ardhi ambayo wako wasdhambuliaji wengi wazuri walitaka kuletwa huku?

Kosa kama hilo la ujuaji pia naliona linaweza kutokea hata pale Yanga kwa mshambuliaji David Molinga mtu ambaye alishika nafasi ya tano katika ufungaji katika ligi yenye wachezaji bora huko DR Congo.

Kuna haja ya kujifunza kupitia matukio haya na kuacha mihemko katika kujadili vipaji vya soka kwa uharaka, hii ni dosari ambayo inataka kuingia ndani ya akili zetu hatua ambayo itazisidi kutupunguzia akili ya kufika katika safari yetu tunayotaka kuianza.

Hebu tusubiri kuona kipi kitaendelea kwa Shiboub na aliyemsajili anywe soda nitakuja kulipa huko aliko aniambie yuko wapi.

Advertisement