Siku za Pochettino Tottenham zahesabika

Muktasari:

Kocha Mauricio Pochettino amebakiza muda mfupi kabla ya kutupiwa virago katika kikosi cha Tottenham Hotspurs.

London, England. Siku za kocha wa Tottenham Hotspurs inayoshiriki Ligi Kuu England Mauricio Pochettino zinahesabika.

Wakati Pochettino akiwa amekalia kuti kavu, makocha watatu Eddie Howe, Julian Nagelsmann na Carlo Ancelotti wanahusishwa kutua White Hart Lane.

Habari za ndani zimedai kuna mazungumzo yanaendelea baina yake na uongozi wa Spurs kuhusu kuvunja mkataba.

Huenda nyota huyo wa zamani wa Argentina akafungashiwa virago muda mfupi ujao.

Matokeo mabaya yameweka rehani kibarua cha Pochetteno ambapo tangu kuanza msimu huu timu hiyo haichezi katika kiwango bora.

Spurs inashika nafasi ya 14 katika ligi ikiwa nyuma kwa pointi 20 dhidi ya vinara Liverpool.

Licha ya Spurs kutolewa katika mtoano kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, vigogo wa klabu hiyo wanamuona Pochettino hatoshi.

Uvumi wa kocha huyo kung’olewa Spurs ulikolezwa na wachezaji mwezi uliopita, lakini alivuka kiunzi hicho.

Licha ya kuonekana hafai Manchester United, Real Madrid na Paris Saint Germain (PSG) inamtolea macho.