Simba kuweka kambi Marekani au Ureno Pre- Season

Muktasari:

Simba imefuzu kucheza Ligi ya Mabingwa kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji amesema kuwa bodi ya wakurugenzi imepanga kuipeleka timu hiyo Marekani au Ureno kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Dewji alisema hayo wakati wa kuipongeza timu hiyo kutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo na zoezi wapi watakwenda itajadiliwa ndani ya wiki hii.

Alisema kuwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo ni mafanikio makubwa ambayo yametokana na ushirikiano baina ya viongozi, wanachama, mashabiki na wadau wa soka kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Dewji, Ligi Kuu ilikuwa ngumu na hasa baada ya klabu ya Yanga ilikuwa inaongoza ligi hiyo kwa pointi 21.

“Haikuwa kazi rahisi kutafuta pointi ambazo wapinzani wetu wameweza kupata. Wachezaji waliweza kupigana kiume mpaka kupata ushindi wakiwa na mechi mbili mkononi.