Wachezaji Simba wapewa likizo siku 4

Tuesday March 20 2018

 

Kikosi cha Simba kilichotua nchini nchini jana Jumatatu kikitokea Misri kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho, kimepewa mapumziko ya siku nne ili kujiandaa na michezo inayofuata ya Ligi Kuu.
Kikosi hicho kitapumzika kwa siku hizo nne kuanzia leo mpaka Ijumaa na Jumamosi kitaanza mazoezi kwa ajili ya  kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara.
Simba imerejea jana Dar es Salaam baada ya kushindwa kufanya vyema kwenye Kombe la Shirikisho, kufuatia suluhu ya bila kufungana dhidi ya Al Masry ya nchini Misri.

Wekundu hao wa Msimbazi wanareje huku wakiwa sambamba na watani zao Yanga kwenye msimamo wa Ligi Kuu baada ya kuwafikia pointi 46 walizonazo.

Advertisement