Siwezi kujihakikishia ushindi, asema Gurdiola

Muktasari:

Hadi sasa Manchester City imeshinda mechi moja kati ya nne zilizopita na tayari inazidiwa kwa tofauti ya pointi tano na vinara wa ligi, Everton.

London, Uingereza (AFP). Pep Guardiola amekubali kuwa hawezi kuwa na uhakika kuwa Manchester City itazinduka kutoka usingizini baada ya Phil Foden kutokea benchi na kuiwezesha kupata sare ya bao 1-1 na West Ham katika mechi ya Ligi Kuu ya soka ya England jana Jumamosi.

Timu ya Guardiola iliruhusu bao katika kipindi cha kwanza wakati Michail Antonio alipoufuata mpira wa juu na kupiga kiki kuandika bao la kuongoza katika Uwanja wa London.

Foden aliingiazwa uwanjani katika kipindi cha pili na akafunga bao la kusawazisha, lakini City haikuweza bao la jingine ugenini kujihakikishia ushindi na sasa imeshinda mechi moja kati ya nne za Ligi Kuu.

City, ambayo imekumbwa na tatizo la majeruhi, ikiwakosa Fernandinho, Aymeric Laporte, Nathan Ake na Gabriel Jesus, ilifikia kwa nadra kiwango chake katika mechi hiyo iliyoongeza matokeo mabovu kwa timu hiyo.

Tayari City iko nyuma ya vinara wa Ligi Kuu, Everton kwa tofauti ya pointi tano, na timu hiyo kutoka jiji la Manchester ilionekana mbovu kuliko wakati wowote tangu Guardiola atue klabu hiyo.

Everton leo Jumapili itakutana na Southampton.

"Mimi si mtu ambaye anaweza kubashiri hali ya baadaye. Tumeshapoteza pointi saba, ambazo ni nyingi,"  alisema Guardiola.

"Tulikuwa na wakati mgumu katika dakika 10 au 15 za kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili tulikuwa vizuri na tulifunga mwanzoni.

"Tulipata nafasi zilizotakiwa kushinda mchezo, lakini bahati mbaya hatukuweza kufunga tena.

"Tumesumbuka sana kwa sababu nyingi. Hatuna budi kujifunza katika kila mechi na kuona nini kitatokea."

Kuongezea katika matatizo ya Guardiola, Sergio Aguero alipata matatizo ya misuli, kwa mujibu wa kocha huyo, ambaye hakujua itamchukua muda gani mshambuliaji huyo nyota kurudi uwanjani.

Aguero hajafunga bao katika mechi za Ligi Kuu tangu Januari na imemchukua muda kurejea katika ubora wake baada ya majeraha.

Akiwa ndio kwanza amerejea uwanjani baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti, mshambuliaji huyo wa Argentina alibadilishwa wakati wa mapumziko na nafasi yake kuchukuliwa na Foden.

Safari ngumu ya kwenda Marseille na baadaye Sheffield United wiki ijayo, itampa mtihani mwingine wa jinsi gani City itatengemeaa kurejea katika ubora wake ulioipa ubingwa mwaka 2018 na 2019.

Baada ya kuzinduka kutoka katika uwezekano wa kulala kwa mabao 3-0 katika dakika kumi za mwisho za mechi iliyopita, haya ni matokeo mengine ya kuridhisha kwa West Ham.

Raheem Sterling alifunga mabao matatu dhidi ya West Ham wakati City iliposhinda kwa mabao 5-0 msimu uliopita na mbio zake kupenya kwa mabeki zilimtengenezea nafasi nzuri Aguero, ambaye shuti lake lilimgonga beki na kutoka nje.

Kwingineko, Fulham ilikubali kipigo cha mabao 2-1 mbele ya Crystal Palace baa ya Riedewald kutangulia kufunga katika dakika ya nane na baadaye Zaha katika dakika ya 64 kabla ya Cairney kuifungia timu yake bao la kufutia machozi katika dakika ya tano ya nyongeza.

Nayo Manchester United iliebndelea kusuasua baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Chelsea kwenye uwanja wa Old Traford, huku Jota akiipa Liverpool bao la ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sheffield United, ambayo ilitangulia kufunga kwa njia ya penati katika dakika ya 13 iliyopigwa na Berge. Bao la kusawazisha la Liverpool lilifungwa na Firmino katika dakika ya 41.

Katika mechi nyingine itakayochezwa leo, Arsenal itaikaribisha Leicester uwanja wa Emirates.

Msimamo wa Ligi Kuu kabla ya mechi za leo Jumapili:

 

Everton                                5 4 1 0 14 7 13

 

Liverpool             6 4 1 1 15 14 13

 

Aston Villa           5 4 0 1 12 5 12

 

Leeds                    6 3 1 2 12 9 10

 

Crystal Palace    6 3 1 2 8 9 10

 

Chelsea                                6 2 3 1 13 9 9

 

Leicester              5 3 0 2 12 8 9

 

Arsenal                 5 3 0 2 8 6 9

 

Wolverhampton               5 3 0 2 5 7 9

 

Tottenham         5 2 2 1 15 8 8

 

West Ham           6 2 2 2 12 8 8

 

Man City              5 2 2 1 8 8 8

 

Southampton    5 2 1 2 8 9 7

 

Newcastle           5 2 1 2 7 9 7

 

Man Utd                              5 2 1 2 9 12 7

 

Brighton               5 1 1 3 9 11 4

 

West Brom         5 0 2 3 5 13 2

 

Burnley                4 0 1 3 3 8 1

 

Sheffield Utd     6 0 1 5 3 9 1

 

Fulham                 6 0 1 5 5 14 1