Solskjaer asema hakuna kama Pogba

Muktasari:

  • Kiwango bora cha mchezaji wa kiungo wa Manchester United Paul Pogba, kimemvutia kocha Ole Gunnar Solskjaer

London, England. Ole Gunnar Solskjaer amemtaja kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba ni mchezaji wa aina yake Manchester United.

Kocha huyo wa muda, alisema Pogba ana kipaji cha soka na juzi alithibitisha ubora wake katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Chelsea.

Licha ya kufunga bao, Pogba alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi.

Kauli ya Solskjaer iliungwa mkono na nyota wa zamani wa timu hiyo Phil Neville aliyesema Pogba ni mchezaji anayevutia kumtazama uwanjani.

Wakati huo huo, nguli wa zamani wa England Alan Shearer amesema Solskjaer ameiweka Man United katika nafasi bora.

Alisema Man United imerejea katika mstari baada ya kufanya vyema katika mechi zake tangu alipojaza nafasi ya Mreno Jose Mourinho.

Kauli ya nahodha huyo wa zamani wa England, imekuja muda mfupi baada ya Man United kuichapa Chelsea mabao 2-0 juzi usiku.

Licha ya kufungwa na Paris Saint-Germain katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki iliyopita, Solskjaer ameshinda mechi 11 kati ya 13.