Solskjaer awambia wachezaji wake tukifungwa na Spurs, Man City nafukuzwa

Tuesday December 3 2019

Solskjaer- awambia -wachezaji - tukifungwa- Spurs-Man City -nafukuzwa-mwananchimichezo-

 

London, England. Ole Gunnar Solskjaer amewaambia wachezaji wake anaweza kufukuzwa kazi kama Manchester United watafungwa na Tottenham Spurs na Manchester City wiki hii.  

Chanzo kutoka ndani ya Manchester United kilisema: 'Ole amekuwa na hofu kidogo juu ya hatma yake na amewaambia wachezaji kama watashindwa kupata matokeo katika mechi hizo mbili wiki hii, basi yeye anaweza kufukuzwa.

'Ni wakati mbaya tunacheza na Spurs wakiwa chini ya Jose.'

Solskjaer imepanda hadi nafasi ya pili ya makocha watakaofukuzwa kwa mujibu wa watabiri hiyo ni kutokana na Manchester United kulazimishwa sare 2-2 na Aston Villa nyumbani Jumapili iliyopita.

Sare hiyo dhidi ya Villa imeifanya Man United kukusanya pointi 18 katika mechi 14, ikiwa ni pointi ndogo zaidi kupata tangu 1988-89, ikiwa ni miaka 31.

Wakati huo, United ilipopata pointi 18 ilimaliza msimu ikiwa nafasi ya 11. Kama watafanikiwa kufikia matokeo hayo ni wazi kutakuwa na nafasi ndogo kwa Solskjaer kuendelea kuiongoza timu hiyo msimu ujao.

Advertisement

Advertisement