Son wa Spurs atoa mabao yake kwa Gomes

Thursday November 7 2019

 

London, England. Nyota wa Tottenham Spurs, Heung-min Son ameonyesha uungana Jumatano katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya Red Star Belgrade na kuzisogelea kamera na kuonyesha ishara ya kumuomba msamaha, Andre Gomes.

Mabao hayo, Son aliyafunga katika mchezo ambao Tottenham iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Red Star Belgrade kwenye Uwanja wa Rajko Mitic.

Mkorea huyo, alisema hakutaka kushangilia kama sehemu ya kusikitishwa na kile kilichotokea kwa bahati mbaya kati yake na Gomes katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu England alimuuiza vibaya bila ya kutegemea.

"Namtakiwa Andre Gomes apone haraka," alisema nyota huyo, akizungumzia tukio hilo kwa mara ya kwanza tangu litokee siku chache zilizopita.

"Nimekuwa na siku ngumu, kiukweli zilikuwa ngumu haswa, lakini kila mmoja amekuwa akinitumia meseji na kutaka niwe jasiri kukubaliana na kilichotokea, nachoweza kusema ni samahani kwa kilichotokea," alisema Son.

Advertisement