Spika wa Bunge awapongeza Simba

Muktasari:

  • Simba imeingia kwenye historia kubwa ya kutinga hatua ya robo fainali kwa kuwafunga As Vita ya Kongo mabao 2-1, mechi hiyo ilipigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Spika wa bunge wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kwa niaba ya wabunge amewapongeza wachezaji, viongozi, mashabiki na Watanzania kwa ujumla Simba kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba imetinga hatua hiyo baada ya kuwafunga AS Vita mabao 2-1 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jambo ambalo spika huyo alidai kitendo hicho kimeleta heshima kubwa kwa Taifa la Tanzania.

"Siyo tu kuandika rekodi kuwa timu ya kwanza Afrika Mashariki kufikia hatua ya robo fainali ya michuano

hiyo, bali kimeleta heshima kubwa kwa nchini yetu.

"Hongera sana wadau wote wa Simba kwa ushindi wenye heshima ya kihistoria kwa taifa dhidi ya wapinzani ambao mlicheza nao," alisema Spika wa bunge, Ndugai.