Stars bado majina tu

Friday August 16 2019

 

By CHARITY JAMES

KIKOSI cha timu ya taifa 'Taifa Stars'  kinatarajia kutajwa muda wowote kuanzia leo, lakini mipango yake ni kuingia kambini Agosti 29 ili kujiandaa na mchezo wa hatua ya awali kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Burundi itakayochezwa Sept 4.

Akizungumza na Mwanaspoti, Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau alisema wamekaa na Kocha Etienne Ndayiragije kupanga mipango yote kuelekea mchezo huo na kubainisha kuwa muda wowote atataja kikosi tayari kwa kuingia kambini.

Kidau alisema wachezaji watakaotajwa katika kikosi cha Stars watatakiwa kuingia kambini mapema kutokana na muda waliono mdogo kuelekea mchezo huo na kuongeza kuwa lengo ni kuona wanapata matokeo.

"Kuna wachezaji wanacheza wapo nje ya Tanzania kama Nahodha Mbwana Samata atakuwa na mchezo Septemba Mosi hivyo ataungana na timu moja kwa moja akitokea Ubelgiji na kwa wengine wataingia kambini kwa wakati mmoja," alisema na kuongeza;

"Katika msafara wa timu ya taifa wataongozana na wahamasishaji waandishi waliojitoa  kuisapoti timu ya wachezaji wa ndani walioitoa Kenya katika mechi za kuwani Cha 2020."

Advertisement