Stars yaanza kazi ya kuikabili Uganda

Muktasari:

Mara baada ya kuwasili kocha mkuu Emmanuel Amunike alifanya mkutano na waandishi wa habari na kubwa ambalo alielezea ni maendeleo ya kikosi chake.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kilifanya mazoezi kwa mara ya kwanza uwanja wa Taifa.
Stars ambao walifika uwanjani hapa saa 10:15 jioni walionekana kuwa na morali huku wachezaji wengi wakionekana na furaha.
Mara baada ya kuwasili kocha mkuu Emmanuel Amunike alifanya mkutano na waandishi wa habari na kubwa ambalo alielezea ni maendeleo ya kikosi chake.
Amunike alisema timu tangu siku ya kwanza inamaendeleo mazuri na kila mchezaji akionekana kuwa na morali ya kushindana.
"Tunaimani tutatimiza lengo la kufuzu kwa kupata matokeo ya ushindi mbele ya mashabiki wa Tanzania," alisema Amunike.
Mara baada ya kumaliza mazungumzo na waandishi wa habari alikwenda uwanjani ili kuanza mazoezi na wachezaji wake.
Kabla ya kuanza mazoezi wachezaji walukusanyika kati kati ya uwanja wakaaomba kisha kuanza mazoezi.
Mazoezi ya kwanza yalikuwa ni kukimbia kwa mwendi wa kawaida huku wakizunguka uwanjani mzima na baada ya hapo walifanya mazoezi ya viungo na yale ya kunyoosha misuli.
Baada ya hapo wakaanza mazoezi ya kupiga pasi ambayo Amunike aliwatenganisha wachezaji katika makundi manne tofauti.
Amunike alitaka kila mchezaji apige pasi kwa mwenzake kwa uharaka.
Wakati mazoezi haya yakiwa yanaendelea Ofisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania Clifford Mario 'Ndimbo' aliwambia waandishi wa habari watoke ndani ya uwanja ili kumuacha Amunike afanye mazoezi na nyota wake.