Sterling afukuzwa kambini kwa utovu wa nidhamu

Muktasari:

  • Kocha Gareth Southgate amemuondoa katika kikosi mshambuliaji  nyota Raheem Sterling kwa utovu wa nidhamu.

London, England. Raheem Sterling ameondolewa timu ya taifa ya England kwa utovu wa nidhamu.

Kocha wa England Gareth Southgate amemtumia Sterling kwa kutaka kuzichapa na mchezaji mwenzake kambini Joe Gomez.

Mshambuliaji huyo alimkaba shingoni Gomez wakati wachezaji wa timu hiyo wakiwa kantini jana mchana.

Tikio hilo limetokea saa chache baada ya wachezaji hao kutaka kuzipiga uwanjani katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Liverpool ilishinda mabao 3-1 katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Anfield.

Habari za ndani zilisema kuwa Gomez alimpa mkono Sterling kwa lengo la kumsalimia lakini, winga huyo alifura na kutaka kumkaba kooni.

Baadhi ya wachezaji walidhani wachezaji walikuwa katika utani kabla ya kubaini Sterling alikuwa amekasirika.

Wachezaji walioshuhudia tukio hilo waliamua mzozo huo na Southgate aliamua kumtimua kambini Sterling.

Kocha huyo amechukizwa kwa utovu wa nidhamu wa Sterling kwa kuwa unaweza kuwagawa wachezaji na kuharibu mipango yake ya mechi yao na Montenegro.

England keshokutwa itavaana na Montenegro katika mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Ulaya.

Licha ya Sterling kumuomba msamaha Gomez na wachezaji wenzake, Chama cha Soka England (FA), kimetoa taarifa ya kuondolewa kambini nyota huyo ambaye amewahi kuvaa kitamba cha unahodha katika baadhi ya mechi.

&&&&&&&&

Kocha Arsenal apewa masharti magumu

S. Kocha wa Arsenal Unai Emery amekweka kitanzi cha kutimuliwa baada ya vigogo wa klabu hiyo kumpa muda hadi mwakani.

London, England. Kocha Unai Emery ameshusha presha baada ya vigogo wa Arsenal kumpa muda hadi mwakani.

Kipigo cha mabao 2-0 ilichopata Arsenal dhidi ya Leicester City, kiliweka rehani kibarua cha kocha huyo.

Idadi kubwa ya mashabiki hawakuliani na mbinu za ufundishaji za kocha huyo na katika mechi za hivi karibuni wamekuwa wakienda uwanjani na mabango.

Pamoja na presha ya mashabiki, vigogo wa klabu hiyo wamempa Emery mechi nne za kujinasua na janga la kutupiwa virago.

Mechi ambazo zitaokoa kibarua chake Southampton, Norwich, Brighton na West Ham United.

Vigogo hao wanaamini mechi hizo zitairejesha timu hiyo katika mstari wa kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

Arsenal itacheza mechi hizo hadi Januari Mosi, mwakani kabla ya kuzivaa Manchester City, Chelsea na Manchester United.

Endapo atavuka kiunzi hicho, kocha huyo wa zamani wa Paris Saint Germain na Valencia anaweza kubaki Emirates.

Wakati Emery akiwa amekalia kuti kavu, baadhi ya makocha nguli wanaotajwa kujaza nafasi yake ni Jose Mourinho, Luis Enrique, Brendan Rodgers na Massimiliano Alegri.