Sterling amtabiria makubwa Sancho

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo alisema ana matumaini Sancho aliyefunga mabao tisa katika mechi 38 alizocheza Dortmund atakuwa mchezaji tishio muda mfupi ujao.

London, England. Raheem Sterling amemtaja mshambuliaji kinda wa Borussia Dortmund Jadon Sancho ni mchezaji wa aina yake.

Mshambuliaji huyo wa Manchester City alisema Sancho atakuwa mchezaji wa aina yake duniani kwa kuwa ana kipaji cha soka.

“Kwa mara ya kwanza baada ya kufanya naye mazoezi, nilibaini ni mchezaji hodari mwenye kipaji,” alisema Sterling.

Mshambuliaji huyo alisema ana matumaini Sancho aliyefunga mabao tisa katika mechi 38 alizocheza Dortmund atakuwa mchezaji tishio muda mfupi ujao.

Wachezaji hao wameitwa katika kikosi cha England kujiandaa na mechi mbili za kufuzu Fainali za Kombe la UIaya dhidi ya Jamhuri Czech na Montenegro.