TFF yapangua kesi, uchaguzi Yanga ndani ya siku saba

Tuesday January 15 2019

 

By THOMAS NG'ITU

Dar es Salaam. Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema itatangaza tarehe ya uchaguzi wa klabu ya Yanga ndani ya siku saba kuanzia jana.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ally Mchungahela alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kukaa chini na kupitia taarifa za wanachama waliopeleka kesi mahakamani siyo wanachama hai.

"Wanachama waliopeleka kesi mmoja tu ndio mwanachama hai, lakini wawili sio wanachama hai kwa hiyo hawana sifa ya kusimamisha uchaguzi," alisema.

Mchungahela aliongeza kuwa waliongea na wanachama hao waweze kufuta kesi hizo mahakamani na wamekubaliana kufanya jambo hilo.

"Katiba ya Yanga, TFF, CAF na Fifa haziruhusu wanachama kupeleka kesi mahakamani bali kesi hizi zinahitajika kumalizwa na TFF kwahiyo wamegeuka katiba," alisema Mchungahela.

Alisema hoja ya kuhusu kadi zitakazotumika katika uchaguzi baada ya mwanachama mmoja aliyesalia kuhitaji kutumika kwa kadi za zamani katika uchaguzi huo licha ya awali kamati hiyo kutangaza kwamba wanachama wote hai wenye kadi tofauti wanaruhusa ya kupiga kura.

Wanachama hao waliofungua kesi walipinga uhalali wa wanachama kadi za zamani CRDB, kitabu na Posta zote kutumika, kukataliwa majina baadhi ya wanachama kuingizwa katika kitabu na sintofahamu ya Mwenyekiti wao kiasi cha wagombea wengine kushindwa kujitokeza kugombea katika uchaguzi huo.

Advertisement