Tanzania kulamba Sh13 bil za FIFA

Wednesday June 13 2018

 

By Charles Abel

Tanzania itapata mgawo wa Dola 6 milioni (zaidi ya Shilingi 13) bilioni kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu.

Rais wa FIFA, Gianni Infantino amethibitisha hilo katika mkutano mkuu wa shirikisho hilo unaondelea muda huu  huko Moscow, Urusi.

Infantino ameahidi kuwa nchi zote 211 kila moja itapata mgawo huo kwa ajili ya kusaidia programu mbalimbali za maendeleo ya mchezo wa soka.

Advertisement