Thompson aiongoza Warriors kuilaza Lakers NBA

Muktasari:

  • Golden State Warriors imeshinda mechi ya nane mfululizo kwenye Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani NBA baada ya kuishinda Lakers iliyokosa nyota wake watatu.

Ustadi wa Klay Thompson wa kufunga kutoka mbali kumeiwezesha Golden State Warriors kupata ushindi wa pointi  130-111 dhidi ya Los Angeles Lakers katika mchezo wa Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani (NBA) jana Jumatatu (Januari 21).
Thompson aliungana na mchezaji mwenzake wa zamani wa Denver Nuggets, Ty Lawson kuwa wachezaji wawili pekee waliofanya majaribio kumi ya kufunga kutokea mbali (three pointer), wakimaliza mchezo huo kwa kufunga mara kumi kati ya 11 kutoka nje ya nusu duara na kwa ujumla mara 17 kati ya 20, wakifunga pointi 44 kabla ya kukaa nje katika robo ya mwisho.
Wakati huo, mabingwa hao watetezi walikuwa mbele kwa pointi 110-80 dhidi ya Los Angeles Lakers, ambayo haikuwa na nyota wake, LeBron James pamoja na Rajon Rondo na Lonzo Ball.
"Pamoja na yote ni ushindi mzuri," alisema Thompson baada ya ushindi huo wa Warriors ambao ni wa nane mfululizo.
Kevin Durant aliongeza pointi nyingine 20 kwa upande wa Warriors na Stephen Curry alifunga pointi 11 na kutoa assist 12, lakini alikuwa ni Thompson aliyeng'ara, akionekana wazi kuondokan a na tatizo lililokuwa likimsumbua la kufunga.
"Wakati unapokuwa na mkono wa moto, unachotafuta ni hata nafasi ndogo --unachotaka ni nafasi ya inchi moja au mbili, hiyo ndiyo inayofanya kiganja kifanye kazi," alisema Thompson. "(Leo) Ilikuwa moja ya siku hizo."
Katika mechi iliyofanyika Philadelphia, mchezaji wa timu ya wenyeji, Joel Embiid alifunga pointi 32 na kupoikonya mipira mipira 14 wakati wenyeji walipokabiliana na james Harden, aliyefunga pointi 37, na kuibuka na ushindi wa pointi 121-93 dhidi ya Houston Rockets.
Hiyo ilikuwa mechi ya 20 mfululizo kwa Harden kufunga pointi 30 au zaidi, lakini Rockets hawakuweza kufua dafu kwa wenyeji. AFP