Tizama kipa mwenye sura mbili

Brussels, Ubelgiji. Thibaut Courtois anaonekana kuwa kipa wa aina tofauti akiwa na timu yake ya Taifa ya Ubelgiji na pale anapoiwakilisha klabu yake ya Real Madrid inayoshiriki Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’.

Courtois alikuwa sehemu ya kikosi cha Ubelgiji ambacho kiliitandika San Marino mabao 4-0 huku mchezo huo ukiwa wanne kwake kucheza bila ya kuruhusu bao.

Lakini imekuwa tofauti pindi akiwa na Real Madrid. Ameruhusu mabao mengi kuliko hata idadi ya michezo ambayo amecheza klabu hiyo, msimu huu wa 2019/20.

Kwenye dakika 360 ambazo amelitumikia Taifa lake ameruhusu bao moja tu, ambalo alifungwa na Mrussia, Denis Cheryshev. Tangu hapo, kipa huyo wa zamani wa Chelsea hajaruhusu nyavu zake kuguswa ndani ya mwaka huu wa 2019.

Amecheza michezo mitano mwaka huu, wameshinda yote huku akiruhusu bao hilo moja kitu kinachowaachia maswali mengi mashabiki wa Real Madri ni kiwango chake akiwa na timu yao.

Lakini awapo Real Madrid, hamna hata mechi moja ambayo hajaruhusu bao. Yaani akiwa Madrid, anakuwa kama shati golini. kila mechi bao.

Mabadiliko