Tottenham Spurs 5-0 Red Stars; Son, Kane wapiga shoo ya kibabe Ligi ya Mabingwa

Wednesday October 23 2019

 

London, England. Wakati Son Heung-min akitangazwa mchezaji bora wa mechi baina ya Tottenham Hotspurs dhidi ya Red Star Belgrade, Mauricio Pochetteno amesifu kiwango cha wachezaji wake.

Heung-min alifunga mabao mawili sawa na nahodha wake Harry Kane katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya waliopata ushindi mnono wa mabao 5-0. Bao jingine lilifungwa na Lamela.

Kocha huyo ambaye amekuwa katika wakati mgumu msimu huu, alitoa sifa kwa wachezaji wake akidai walicheza kwa kiwango bora.

Pochettino amewataka wachezaji wake kulinda viwanga vyao katika mechi zijazo za mashindano.

Matokeo hayo yanaweza kuiweka Spurs katika nafasi nzuri inapojiandaa kwa mchezo ujao dhidi ya Liverpool. Spurs imepata ushindi wa kwanza katika mechi nne zilizopita.

“Ni muhimu kwetu kulinda kiwango hiki. Tumejifunza kitu kipya na kupata uzoefu mpya. Nina furaha haya ni matokeo mazuri nadhani huu ni muda mzuri wa kurejea katika ubora wetu,”alisema Pochettino.

Advertisement

Kocha huyo Muargentina alidai hakuwa na kikwazo kwa wachezaji wake baada ya kuomba siku moja ya kupumzika.

Kane alisema ushindi huo utawaweka katika mstari wa kurejesha makali yao katika mechi zijazo.

 

 

Advertisement