Tshishimbi afunguka kufanya kazi na kocha Mkwasa

Muktasari:

  • Tshishimbi alipewa unahodha chini ya kocha Mwinyi Zahera ambaye hivi karibuni alitimuliwa na uongozi wa Yanga.

Dar es Salaam.Nahodha na kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi amesema wataendelea kupambana na kutoa ushirikiano wote kwa kocha wao mpya Charles Mkwasa na benchi lake la ufundi.

Tshishimbi alisema pamoja na kuondoka kwa kocha Mwinyi Zahera na mabadiliko ya benchi la ufundi, kilichowaleta Yanga ni kufanya kazi na kuipa mafanikio Yanga.

"Kama tupo Yanga ni kwa ajili ya kufanya kazi na si vingine. Sisi tutapambana muda wote kuona tunaifanya Yanga kufikia malengo yaliyokusudiwa,"alisema Tshishimbi.

Alisema, wanachotakiwa kufanya ni kujituma na kuweka malengo kwa kila jambo huku wakimshirikisha Mungu watafanikiwa.

Yanga sasa ipo chini ya kocha wa muda, Boniface Mkwasa akisaidiwa Said Maulid 'SMG'.