Ujio wa Sevilla watikisa maandalizi Simba

Thursday May 16 2019

By Majuto Omary

Dar es Salaam. Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limesema kuwa ujio wa timu ya Sevilla kutoka nchini Hispania chini ya udhamini wa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa Tanzania utaongeza hamasa na maendeleo ya mpira wa miguu nchini.

TFF pia imewataka wachezaji wa Simba kutumia fursa ya mechi hiyo kuonyesha na vipaji vyao. Mechi hiyo itaonyeshwa na DStv kupitia Supersport 9.

Timu ya Sevilla FC inatarajiwa kuwasili Tanzania Mei 21 na baadaye kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu ya Simba Mei 23 kwenye uwanja wa Taifa kuanzia saa 1.usiku.

Rais wa TFF, Wallace Karia alisema kuwa Sevilla FC ni timu kubwa yenye historia kubwa katika soka duniani na hivyo ujio wao utawavutia mashabiki wa soka hata wan chi jirani ili kuja kushuhudia wachezaji nyota wa wanaocheza bara la Ulaya.

Karia alisema kuwa ni historia kwa Tanzania kwani tangu mwaka 2017, kampuni ya SportPesa imekuwa ikileta hamasa kubwa kwa mashabiki wa soka, wachezaji , viongozi na makocha kutokana na shughuli mbalimbali za kimichezo zilizofanikishwa na kampuni hiyo.

“Walianza na ujio wa timu ya Everton ambayo ilicheza mechi kwenye uwanja wa Taifa dhidi  ya timu ya Gor Mahia ya Kenya. Mastaa kama Wayne Rooney na wengine kibao walicheza kwa mara ya kwanza Tanzania na kuleta hamasa,” alisema Karia.

Alifafanua kuwa Sevilla FC ni mabingwa mara nyingi wa michuano ya Europa na ujio wao utaongeza hamasa iliyoanzishwa na Everton hapa nchini.

 Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa Tanzania,Tarimba Abbas alisema kuwa wanajivunia kuwa wadau wa kweli wa maendeleo ya mpira wa miguu nchini na kuwaomba mashabiki wa soka kujaa uwanjani kushangilia timu ya Simba.

Tarimba alisema kuwa lengo la SportPesa Tanzania ni kuona kila Mtanzania anapenda mchezo wa soka na kutokana na hilo wameweka viingilio vya Sh5,000 na Sh15,000 ili kuwavutia mashabiki na kuujaza uwanja huo. Pia kutakuwa na kiingilio cha Sh100,000 kwa upande wa viti maalum.

Alisema kuwa kwa kuzingatia hilo, wameamua kuanzisha promosheni ya “Usibahatishe Cheza na SportPesa”  ambayo mbali ya washindi kuzawadfia gari aina ya Toyota IST tatu, pia watatoa tiketi 45 kwa washindi ili kuona mechi hiyo.

Majuto Omary

Advertisement