VAR yabariki ushindi wa Manchester United kwa Chelsea

Muktasari:

Chelsea inakuwa timu ya pili kupata mabao yake mawili hali, lakini VAR inakataa ya kwanza ilikuwa Sheffield United dhidi ya Brighton mwezi Desemba.

London, England. Kocha Frank Lampard amesema matumizi ya teknoloji ya waamuzi video haikutenda haki kwa Chelsea ikichapwa nyumbani mabao 2-0 na Manchester United na kuacha majonzi makubwa kwa mashabiki wa Blues.
Msimamizi wa VAR, Chris Kavanagh hakuona kama Harry Maguire anastahili kupewa kadi nyekundu kwa kumkanyaga kusudi Michy Batshuayi.
Kavanagh pia alikataa mabao mawili ya Chelsea moja akidai kuna mtu amesukumwa na nyingine ni kuotea.
Mamia ya mashabiki wa Chelsea waliondoka kwenye Uwanja wa Stamford Bridge zikiwa zimebaki zaidi ya dakika 10.
Bao la kichwa la Anthony Martial na lile la Maguire yametosha kuihakikishia Manchester United ushindi wa pili mfululizo katika Ligi Kuu dhidi ya Chelsea ikiwa ni mara ya kwanza tangu msimu wa 1987-88.
Chelsea inakuwa timu ya pili kupata mabao yake mawili hali, lakini VAR inakataa ya kwanza ilikuwa Sheffield United dhidi ya Brighton mwezi Desemba.
Akizungumzia tukio hilo Lampard: "Nimetazama tena na VAR ilikuwa pale kufanya kitu ambacho si sahihi. Harry Maguire alistahili kutolewa kwa kadi nyekundu, ilikuwa wazi na hiyo ingetosha kubadili hali ya mchezo."
Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer: "Je ni kweli Harry Maguire ni mwenye bahati? Sidhani kama ni hivyo. Alianza kuchezewa faulo kwanza na Batshuayi alipotaka kumwangukia alijaribu kujizuia kwa kuinua mguu na bahati mbaya ulimpata sehemu iliyomuuza."
Maguire: "Nilijua kuwa nilimgusa alianza kuanguka ni kawaida kwa mtu kujitetea kwa kumzuia ndipo mguu wangu ukamzuia. Naomba msahama kwake na vizuri kwa mwamuzi alitambua jambo hilo."
Manchester United imepanda hadi nafasi ya saba na kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.

Manchester United sasa ipo nyuma kwa pointi tatu kwa Chelsea inayoshika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu England.