VIDEO: Makambo alivyowasili usiku,Presha yashuka Yanga

Wednesday January 16 2019

By Naheka Khatim

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo amewasili nchini leo alfajiri akitokea DR Congo ambako alikwenda kushughulikia masuala ya kifamilia.

Makambo ambaye anaongoza kwa ufungaji kwa klabu yake ya Yanga alirudi kwao mara baada ya mechi ya mwisho ya timu yake dhidi ya Mbeya City  mwishoni mwa mwaka jana na sasa amerejea kuendelea na klabu yake.
Mshambuliaji wa Yanga Haritier Makambo amerejea rasmi na kuwashusha presha mashabiki na viongozi wa klabu yake lakini alichelewa kurejea kwa siku mbili  zaidi na na hali hiyo kusababisha zikasambaa taarifa kudai ametoroka.


Hata hivyo jana mara baada ya Yanga kucheza dhidi ya Mwadui kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alikanusha taarifa za Makambo kutoroka akisema habari hizo hazina ukweli.
Akizungumza mara baada ya kuwasili Makambo amesema amerejea kazini na wala hakutoroka kama ilivyodaiwa.
Mshambuliaji huyo amesema kuondoka kwake kulikuwa na ruhusa maalum kutoka kwa Zahera na uongozi na kwamba alikwenda kushughulikia matatizo ya familia yake

Advertisement