VIDEO: Msuva: Taifa Stars itafuzu kwa Afcon2021 Cameroon

Muktasari:

  • Msuva ametua nchini akiwa ametoka kuisaidia klabu yake ya Difaa kuibuka na ushindi katika mchezo wa mwisho wa Ligi dhidi ya Rabat ambao walishinda kwa mabao 3-1 huku akifunga mawili.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Difaa El Jadida ya Morocco, Saimon Msuva anaimani timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itafuzu kwa mara nyingine kucheza  fainali za Mataifa ya Afrika Afcon 2021 Cameroon.

Taifa Stars itaanza kampeni za kuwania kufuzu kwa Afcon, Novemba 15 kwa kucheza na Guinea ya Ikweta.

Msuva aliyetua nchini leo akitokea Morocco, alisema uzoefu wa awamu iliyopita utakuwa sehemu ya wao kufanya vizuri katika kampeni ya Afcon 2021.

"Hatuanzi upya tunaendelea tulipoishia, tutapambana kama timu ambayo inaujua utamu ya kucheza Afcon," alisema Msuva.

Msuva aliongeza,"Kikubwa ni Watanzania kutusapoti, kila mchezo ambao tutakuwa nyumbani, tujitokeze na kuujaza uwanja, itatupa nguvu kwa wachezaji."

Mwaka 2019 fainali za Afcon zilifanyika nchini Misri, Tanzania ilishiriki kwa mara ya pili na kuishia katika hatua ya makundi.