Vigogo Afrika wapata matokeo mazuri Ligi ya Mabingwa

Monday September 16 2019

 

By AFP

Wakati viogogo vya soka barani Afrika vikiaqnza vyema mechi za kwanza za raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa, timu kutoka ukanda wa Afrika Mashariki zimejiweka katika nafasi ngumu ya kuingia hatua ya makundi.

Mabingwa watetezi Esperance kutoka Tunisia wameanza kampeni ya kutaka kuwa klabu ya kwanza Afrika kutwaa kombe la Ligi ya Mabingwa wa soka mara tatu mfululizo kwa kutoka sare bya bao 1-1 ugenini na Elect-Sport ya Chad jana Jumapili.

Wababe wa Simba, TP Mazembe pia walilazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji Fosa Juniors jijini Mahajnga, Madagascar, matokeo ambayo pia walipata mabingwa wengine wa zamani Enyimba nyumbani mbele ya El Hilal ya Sudan.

Vigogo Al Ahly ya Misri walianza vizuri zaidi kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cano Sport ya Equatorial Guinea, Raja Casablanca wakiibuka na ushindi mnonowa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Al Nasr ya Libya, huku Zamalek wqakipokea kichapo cha mabao 2-1 mbele ya wenyeji  Generation Foot ya Senegal mjini Thies.

Katika ukanda wa Afrika Mashariki, Gor Mahia ya Kenya walifungwa mabao 4-1 ugenini na USM Alger ya Algeria huku KCC ya Uganda ikilazimisha sare ya bila kufungana na Petro Atletico ugenini jijini Luanda, na Yanga ikilazimishwa sare ya bao 1-1 jijini Dar es Salaam na Zesco ya Zambia.

Jijini Djamena, Fedi Ben Choug aliwafungia Esperence bao la kuongoza katika dakika ya 66 na Haroun Bokhit akasawazisha kabla ya mchezaji mwenzake, Leger Djimrangar kupoteza penalti katika mechi hiyo.

Advertisement

Esperance ilikosa wachezaji wengi nyota ambao waliiongoza timu hiyo kutetea ubingwa katika mazingira mabovu, akiwemo Youcef Belaili wa Algeria ambao wamejiunga na klabu nyingine.

Winga Belaili, mmoja wa wachezaji waliokuwa kwenye kikosi cha Algeria kilichotwaa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu, amejiunga na Al Ahly Jeddah ya Saudi Arabia.

Beki wa kushoto Ayman Ben Mohamed amesaini kuichezea klabu ya Le Havre ya Ufaransa, kiungo Ghaylen Chaaleli ameenda Malatyaspor ya Uturuki na mshambuliaji Saad Bguir ameenda Abha ya Saudi Arabia. 

Baada ya kupata tiketi ya kuvuka raundi ya awali mezani, Esperance inaonekana kuwa na uhakika wa kupata ushindi w ajumla dhidi ya Elect wakati timu hizo zitakapokutana tena mwezi huu nchini Tunisia.

Esperance ilidhani imeshatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa mwaka 2019 mapema Juni mosi wakati wapinzani wao katika mechi ya fainali walipovamia uwanja kupinga uamuzi wa refa wa kukataa goli.

Kutofanya kazi kwa mashine ya refa msaidizi, VAR kulisababisha kushindwa kuhakikisha kama kulikuwa na rafu kabla ya Wydad kuamini wamesawazisha bao katika mechi hiyo ya marudiano na hivyo kuibuka bingwa kwa jumla ya mabao.

Baada ya mechi hiyo kuchelewa kwa dakika 90, Esperance walipewa ubingwa na medali, lakini Shirikisho la Soka Afrika (CAF) likaagiza mechi hiyo irudiwe kwenye uwanja usio na mwenyeji.

Klabu zote zilipinga maagizo hayo na kukata rufaa Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo, ambayo iliamua kuwa kamati ya nidhamu ya CAF ndiyo iliyotakiwa kufanya uamuzi na si kamati ya utendaji. Kamati ya nidhamu ikaipa ushindi Esperance na hivyo kuifanya klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Afrika mara nne (1994, 2011 na 2018).  

Matokeo ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika za mwishoni mwa wiki:

Mjini Cairo: Al Nasr (Libya)                           1 Raja Casablanca (Morocco) 3

Mechi ilihamishiwa Misri kutokana na sababu za kiusalama

Jijini Lome: ASC Kara (Togo)                        0 Vita Club (Congo)         0

Jijini Aba: Enyimba (Nigeria)                        0 Al Hilal (Sudan)                              0

Jijini Blida:USM Alger (Algeria)   4 Gor Mahia (Kenya)      1

Jijini Kumasi: Asante K (Ghana)  2 Etoile Sahel (Tunisia)   0

Jijini Nouakchott: Nouadhibou (MTN)    0 W. Casablanca (Morocco)         2

Jijini N'Djamena:Elect-Sport (Chad)         1 Esperance (Tunisia)     1

Jijini Mahajanga: Fosa J.(Madagascar) 0 TP Mazembe (COD)        0

Jijini Algiers: JS Kabylie (Algeria) 2 Horoya (Guinea)                           0

Jijini Malabo:Cano Sport (Guinea)            0 Al Ahly (Misri)                2

JijiniThies:Generation Foot (Senegal)     2 Zamalek (Misri)                             1

Jijini Luanda:Petro Atletico (Angola)        0 KCC (Uganda)                 0

Jijini Victoria: Cote d'Or (Seychelles)        0 Mamelodi (Afrika Kusini)           5

Jijini Dar es Salaam: Yanga                            1 Zesco Utd (Zambia)     1

Jijini Bulawayo:Platinum (Zimbabwe)      1 Songo (Msumbiji)                         0

Jijini Lusaka: Green Eagles (Zambia)         1 Primeiro Agosto (Angola)          2

Advertisement