Vigogo Man United wamkingia kifua Solskjaer

Muktasari:

Licha ya kufanya vibaya katika mechi za Ligi Kuu England kibarua cha kocha Ole Gunnar Solskjaer kipo salama baada ya vigogo wa Manchester United kumkingia kifua.

London, England. Kibarua cha kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer licha ya kuboronga katika mechi za Ligi Kuu England msimu huu.

Taarigfa ya klabu hiyo imekuja siku chache baada ya Man United kulala mabao 2-0 dhidi ya watani wake wa jadi Liverpool kwenye Uwanja wa Anfield, Jumapili.

Badala yake kocha huyo ameahidiwa na bodi kupewa fungu la usajili wa dirisha dogo na majira ya kiangazi kwa lengo la kuboresha kikosi hicho.

Man United imekosa nafasi ya kucheza Ligi ya Europa, lakini mabosi wa klabu hiyo wanamuona Solskjaer anastahili kuendelea na kibarua.

Klabu hiyo ipo mbioni kukamilisha usajili wa nahodha wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes ambaye kwa mudam mrefu alikuwa akitakiwa na kocha huyo.

Taarifa hiyo inaonyesha kocha wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino aliyekuwa akisubiri simu ya Man United atalazimika kusubiri.

Mtendaji Mkuu na Makamu Mwenyekiti wa Man United, Ed Woodward na wamiliki familia ya Glazer wameendea kumbeba kocha huyo licha ya kupigiwa kelele za kutakiwa kuondoka.

Mchambuzi Gary Neville ni miongoni mwa nyota wa zamani wa klabu hiyo ambao wamekuwa mstari wa mbele kutaka Woodward aondoke Old Trafford akidai ndiye chanzo cha kufanya vibaya.