Wanachama Simba kupendekeza jina la uwanja

Kesho Jumapili, klabu ya Simba inafanya mkutano mkuu wa mwaka ambapo wanachama wamepewa nafasi ya kupendekeza jina la uwanja wao uliopo Bunju B nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Hayo yamesema na Msemaji wa klabu hiyo Haji Manara wakati wa kuwaonyesha wanachama wao maendeleo ya uwanja wao ambao utaanza kutumika kwa ajili ya mazoezi na Januari mwakani utazinduliwa ramsi.
"Kwenye mkutano ndiko kutapendekezwa jina la uwanja huu kwamba utaitwaje hivyo tusubiri hiyo kesho (Jumapili), hii ndiyo Simba inayowajali wanachama wake," amesema Manara
Simba imejenga viwanja viwili Bunju ambapo kimoja ni cha nyasi bandia kingine nyasi za kawaida ambapo sasa timu yao itaanza kufanya mazoezi na kupunguza gaharama za kulipia viwanja vya mazoezi ambapo sasa hutumia uwanja wa Gymkhana.
Mbali na uwanja wa Gymkhana pia walikuwa wanatumia uwanja wa Boko Veterani ambapo viwanja vyote ni vya kukodi.