Wanasoka wanaopewa uraia China kuongeza nguvu kufuzu Kombe la Dunia

Muktasari:

Tayari klabu zimesajili wachezaji tisa wa kigeni ambao wameomba uraia wa China na ,,oja ameshacheza mechi mbili

China inaweza kuanza kutumia kwenye timu ya taifa wanasoka ambao hawana asili ya nchi hiyo baada ya mamlaka kusema wachezaji tisa wa kigeni wanapewa uraia.
Jumatano, mshambuliaji mzaliwa wa Brazili, Elkeson alikuwa mchezaji wa kwanza ambaye hana asili ya China kuitwa timu ya taifa, ikiwa ni katika kipindi ambacho taifa hilo linataka kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya pili.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 anatarajiwa kuchezea China kwa mara ya kwanza katika mechi ya awali ya Kombe la Dunia mjini Maldives, ambako mchezaji chotara ambaye ni mzaliwa wa London, anatarajiwa kuichezea nchi hiyo kwa mara ya tatu.
"Tunataka kwenda Qatar (kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022)," alisema Chen Xuyuan, rais mpya wa Chama cha Soka cha China (CFA), akikaririwa na vyombo vya habari.
"Wachezaji wanaopewa uraia wanaweza kuwa msaada mkubwa katika kufikia malengo ya muda mfupi ya timu ya taifa.
"Hadi sasa, klabu zimesajili wachezaji tisa waliopewa uraia ambao wana asili au hawana asili ya Uchina, baadhi yao bado wapo kwenye mchakato wa kupewa uraia."
Chen, named to the top post in Chinese football on Thursday, said that more naturalised players will likely represent China as qualification for 2022 progresses.
"Lakini haitakuwa sera ya muda mrefu ya CFA na idadi itakuwa ndogo sana," shirika la habari la Xinhua lilimkariri kiongozi huyo.
Washambuliaji kadhaa wa Kibrazili wanaocheza Ligi Kuu ya China wameripotiwa kuwa miongoni mwa walioomba uraia, kama ilivyo kwa beki mzaliwa wa Uingereza, Tyias Browning.
Lakini uamuzi wa kuwapa hati za kusafiria wachezaji waliozaliwa nje ya nchi -- hasa wasio na asili ya China -- umegawanya mashabiki.
Baadhi wanasema CFA haina budi kufanya kila iwezalo kukisaidia kikosi cha taifa kinachofundishwa na Marcello Lippi kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya pili.
Wengine wanasema nchi yenye watu bilioni 1.4 inatakiwa ifanye kazi nyepesi ya kupata wachezaji kumi na moja wazuri.
China ilifikia fainali hizo kubwa katka soka duniani mwaka 2002, lakini ikamaliza bila ya kupata hata pointi moja au kufunga bao.
Rais Xi Jinping anataka China kuwa taifa kubwa katika soka duniani ifikapo mwaka 2050, lakini timu hiyo inayofundishwa na Lippi inashika nafasi ya 71 katika orodha ya ubora ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa).
Chen pia alirudia kueleza tena nia ya China kuandaa fainali za Kombe la Dunia, moja pia ya mipango ya Xi kwa soka la nchi hiyo.
"Kuandaa Kombe la Dunia ni ndoto ya mashabiki wote wa China, nikiwemo mimi," alisema Chen, akikataa kusema muda ambao nchi hiyo itatekeleza nia hiyo.
"CFA itachambua na kuangalia ni muda gani unafaa kuwasilisha maombi," aliongeza.