Watanzania wakesha mitandao kusubiri usajili wa Samatta, Aston Villa

Dar es Salaam.Watanzania wamekesha katika mitandao ya kijamii ya Instagram na Twitter kufuatilia kwa karibu kurasa za mitandao ya kijamii za Club ya Aston Villa kutaka kujua hatma ya mshambuliaji Mbwana Samatta kujiunga na klabu hiyo ya England.
Watumiaji hao wa mitandao wamekuwa wakivamia kila aina ya Post inayowekwa katika kurasa hizo wakishinikiza kuwekwa kwa picha ya Mtanzania huyo ambaye inaelezwa yupo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wake na Aston Villa.
Taarifa za Samatta kusajiliwa na Aston Villa ziliwekwa wazi Alhamis ya wiki hii na kuamsha shangwe na furaha miongoni mwa Watanzania wanaofuatiklia soka huku wengi wakitamani kuona suala hilo
Matamanio ya wengi ni kuona Samatta anakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Kuu England inayotajwa kuwa ndio ligi maarufu kwa sasa duniani
Taarifa ambazo siyo rasmi hadi jana Ijumaa zilidai kuwa Samatta alikuwa akifanyiwa vipimo vya afya kama hatua ya mwisho ili kutambulishwa rasmi huku ikisubiriwa taarifa rasmi kutoka Aston Villa kuhusu usajili huo
Katika muendelezo wa Ligi kuu England leo Aston Villa itacheza dhidi ya Brighton & Hove Albion ambapo wameweka tangazo la mchezo huo katika mitandao yao ya kijamii, lakini wamejikuta wakipata michango ya watanzania wakishinikiza kutangazwa kwa Mbwana Samatta.
Katika post yao Aston Villa wameandika :M A T C H D A Y ! ambapo michango ya watu mbalimbali imekuwa ni kushinikiza kutangazwa kwa Samatta


edwardchristopher001
And what about @samagoal77 πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™


felichism_mrosso
All the best guys waiting for official news from our beloved @samagoal77
Tunamtaka @samagoal77
khalidi_salym
Sammata sammatta sammata we need to see @samagoal77 right now πŸ€’πŸ€’πŸ€’πŸ€’ post him ebooooo😎😎😎

hussein__karuki
Mr ADIMIN FANYA KUWEKA PICHA YA @samagoal77 UEPUKE COMMENTS ZA WABONGO πŸ˜‚πŸ˜‚
thisispray
Oya wanangu mbona Mnakaa kimya sana Wajubaa mtangazeni basi mwamba @samagoal77

iamsimoneriyo
ALAFU HAWA JAMAA MBNA WANATAKA TUWATUKANE WAMTOE MCHEZAJI WETU KWA MKOPO πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
realcostantine_lenhardt
Chairman wa @avfc ametangaza ati kila Mtanzania alieye follow account zao kulamba dola 1850 maana wamefurahi sana kupata followers wengi kwa siku moja hasa kutokaπŸ‡ΉπŸ‡Ώ.
castortonyasimbadamu
oya nyie watu mbona tangia jana hamumtangazi samatta? wakati tushajua kuwa kasinya kwenu?

sixflying_dragons
Napita kwa kunata

gozbat3
Wolikam samattaa tazanniya πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ‘
hussein__karuki
NIKIJISIKI KUWA HAPPY NAPITA HUKU...
barickthomas118gmail.com2
Welcome Tanzania Aston Villa πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡Ώ
jay_wa_msimamo
TUNAMTAKA MBWANA ALLY SAMATTAπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡Ώ
15h2 likesReply
hendrishalexander
@samagoal77 our great hero of πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ’ͺ
willydosage
Uyu boya anapna raha wabongo wanavyojaza koment πŸ˜‚

hassanmansury13
Hapa hata @avfcofficial wanashangaa leo page yao ghafla imeongezeka followers na Comment na hapo bado haijawa officialπŸ˜‚πŸ˜‚Wabongo tunatisha
alpha_mhoga
Huko kwenu sangapi? Tuwekeeni mtu na nusu basiπŸ˜€ #mbwana Samatta
kamili_africa
ANNOUNCE THE AFRICAN PRINCE πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ€΄πŸΎπŸ‡ΉπŸ‡Ώ
jay_wa_msimamo
MBWANA ALLY SAMATTA

amosymkuta
Oya nyie tutawatukana mjue mbona hamumitangazi @samagoal77 ??
edokumwembe
Yaani kosa lao kumtaka Samatta mpaka wanatukanwa hivi? Wabongo process za mwisho zina mambo mengi aisee... Medical, apigwe picha, afanye mahojiano na TV ya klabu, website na mengineyo... Hii sio Simba na Yanga zetu tulizozoea... Punguzeni jazba kidogo wadau πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
hendrishalexander
We need the post of our @samagoal77 the king of πŸ‡ΉπŸ‡Ώ
godfreymuge
Tuwe wavumilivu sisi wa Tanzania, captain wetu Atatangazwa tu #Samagoli&Aston villa fanyeni kweli apo mmepata mtu sahihi aiseeπŸ‘πŸ‘πŸ‘β€